Banza Stone afunguka Baada ya Kuzushiwa Kifo

Thursday, June 25, 2015

Nkupamah blog

Baada ya kuzushiwa kifo ,muimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Banza Stone amesema si jambo la busara la kuzushiana kifo
 
Akizungumza kwenye AMPLIFAYA   ya  Clouds  Fm jana june 24 alisema: "Mimi nilikuwa nasumbuliwa na kichwa sana na ki homa homa fulani kama miezi miwili lakini saaa hivi niko vizuri, naendelea poa na leo nilienda hospitali daktari kufanya sound check akaniambia kuwa malaria"
 
Mtangazaji:…Jana ilikua ni mara ngapi kuzushiwa kifo ?
 
Banza Stone:.."Mimi hata sijui ila nasikia mara watu oooh banza kafa, mara ooh kila mtu anaongea lake ila mimi niko poa ni mzima naweza kufanya kazi ila kwasasa siko tayari kufanya kazi kwani nitauchosha mwili mwangu"
 
Mtangazaji: Vipi kuhusu kazi zako za muziki bado unaendelea nazo ama au ??
 
Banza Stone:….."Naweza kusema ninaendelea na muziki kama kawaida kwasababu sasa hivi nina kama nyimbo sita  mpya ziko ndani kesho, kesho kutwa naweza nikaamua niachie moja mpaka video ziko tayari sio za bendi bali ni  zangu binafsi…"
Nkupamah blog
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment