- Written by Nkupamah blog
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi
akiwasili kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kupokelewa na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub huku Meya wa Manispaa ya Iringa
Amani Mwamwindi akishuhudia.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub (kushoto) akitoa taarifa migogoro
ya ardhi inayoukumba Mkoa huo na utekelezaji wake.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub akitoa taarifa migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo na utekelezaji wake.
Wakuu wa
vyombo vya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Iringa wakifuatilia kwa kina
taarifa ya migogoro iliyokuwa ikisomwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa
Iringa, Wamoja Ayoub (hayupo pichani).
Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi akizungumza katika kikao hicho kilichowashirikisha watendaji wa mkoa wa Iringa.
Ofisi za
NHC mkoa wa Iringa kama zinavyoonekana leo hii, ambapo Waziri Lukuvi
alitembelea na kuagiza Shirika la Nyumba nchini kuhakikisha kuwa
linaboresha mazingira ya Manispaa ya Iringa kwa kuhakikisha kuwa
linajenga nyumba bora, pia aliagiza Shirika hilo kufanya utafiri ili
liweze kujenga nyumba za gharama nafuu zaidi ili ziwanufaishe wananchi
wengi zaidi.
Meneja
wa NHC mkoa wa Iringa, Humphrey Kishimbo akitoa taarifa ya utendaji ya
NHC mkoa wa Iringa kwa Waziri Lukuvi wakati Waziri huyo alipotembelea
Shirika hilo leo asubuhi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza
akifutilia taarifa hiyo.
Baadhi
ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na wale wa mkoa wa Iringa
wakifuatilia taarifa ya utendaji wa Shirika iliyokuwa ikitolewa na
Meneja wa NHC mkoa wa Iringa, Humphrey Kishimbo (hayuko pichani).
Baadhi
ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na wale wa mkoa wa Iringa
wakifuatilia taarifa ya utendaji wa Shirika iliyokuwa ikitolewa na
Meneja wa NHC mkoa wa Iringa, Humphrey Kishimbo (hayuko pichani).
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi
akizungumza na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na wale wa
sekta ya ardhi na Sekretarieti ya Mkoa wa Iringa ambapo
alisisitiza Shirika la Nyumba nchini kuhakikisha kuwa linaboresha
mazingira ya Manispaa ya Iringa kwa kuhakikisha kuwa linajenga nyumba
bora, pia aliagiza Shirika hilo kufanya utafiri ili liweze kujenga
nyumba za gharama nafuu zaidi ili ziwanufaishe wananchi wengi zaidi..
Baadhi
ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na wale wa mkoa wa Iringa
wakifuatilia taarifa ya utendaji wa Shirika iliyokuwa ikitolewa na
Meneja wa NHC mkoa wa Iringa, Humphrey Kishimbo (hayuko pichani).
Ofisi
za NHC mkoa wa Iringa kama zinavyoonekana leo hii, ambapo Waziri Lukuvi
alitembelea na kuagiza Shirika la Nyumba nchini kuhakikisha kuwa
linaboresha mazingira ya Manispaa ya Iringa kwa kuhakikisha kuwa
linajenga nyumba bora, pia aliagiza Shirika hilo kufanya utafiri ili
liweze kujenga nyumba za gharama nafuu zaidi ili ziwanufaishe wananchi
wengi zaidi.
Waziri
Lukuvi akikagua mafaili yaliyopo katika masjala ya Ardhi ya Halmashauri
ya Manispaa ya Iringa ili kujionea utendaji wa wanfyakazi wa kitengo cha
ardhi.
Waziri
Lukuvi akionyeshwa Master Plan ya Manispaa ya Iringa ambayo iko katika
mchakato wa kukamilika kwaajili ya kuanza kutumika kuupanga vyema mkoa
huo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi
akiongea na wananchi waliojitokeza kuwasilisha kero zao katika ukumbi wa
Siasa ni Kilimo mkoani Iringa. Alisisitiza kuwa Mkoa wa Iringa
uharakishe kupima ardhi ya wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Sehemu
ya umati wa wananchi wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri Lukuvi
aliposikiliza kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Manispaa ya
Iringa.
Sehemu
ya umati wa wananchi wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri Lukuvi
aliposikiliza kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Manispaa ya
Iringa.
Sehemu ya
umati wa wananchi wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri Lukuvi
aliposikiliza kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Manispaa ya
Iringa
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi
ameanza ziara ya siku tatu Mkoani Iringa ambapo aliongea na watendaji wa
Mkoa wa Iringa kuhusiana na migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo .
Aidha, Waziri Lukuvi alipata fursa ya kukagua shughuli za Shirika la
Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi
wa Manispaa ya Iringa na wilaya za jirani za Kilolo na Mufindi. Katika
ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake aliyoitoa katika mikoa
aliyokwishafanya ziara kwa kuwaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima,
wathamini na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa
kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi. Aidha ameutaka Uongozi wa Mkoa
wa Iringa kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na utoaji wa hati na
kutenga muda wao ili kuweza kusikiliza kero za wananchi ili kupunguza
migogoro ya ardhi.
0 comments :
Post a Comment