Thursday, June 25, 2015
Nkupamah blog
Mtangazaji mwenye sauti nzito Bongo kupitia Clouds FM, Millard Ayo, Jumatatu iliyopita alibanwa azungumzie uhusiano wake na warembo wenye majina makubwa nchini, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambapo alimfungukia mmoja mmoja.
Katika
mahojiano maalum na Kipindi cha Sporah Show, mtangazaji alimbana
Millard akimtaka aseme ukweli kuhusu warembo hao ambapo alianza kwa
kumzungumzia Lulu kuwa hajawahi kuwa mpenzi wake zaidi ya kumfahamu
katika sanaa.
“Kuhusu
Lulu! Hapana sijawahi kabisa kuwa na uhusiano naye. Yaani hata kuwaza
sijawahi. Namfahamu kuwa ni mwigizaji na ni mtu ambaye nimekuwa
nikimfuatilia kupitia kazi zangu za utangazaji,” alisema mtangazaji huyo staa.
Millard aliendelea kupangua, ikafika zamu ya Wolper. Alikana vikali kuwa naye hata kujuana kwao si kwa ukaribu. Alisema:
“Haa!
Wolper ndiyo kabisa, nimekuwa nikimuona na kumsikia tu, wala sikuwahi
kumuwazia kwa lolote lile isipokuwa ninamjua kama msanii wa Bongo Muvi
na huwa nakutana naye kama ninavyoweza kukutana na mtu mwingine yeyote
ambaye hatujuani.”
Kwa
upande wa Jokate, hapo alipiga kituo kidogo na kuanza kumzungumzia
kwamba, amemfahamu miaka mingi na alikuwa akimpenda kama ‘girl friend’
wake kwani wakati anasoma alishawahi kupanda naye daladala na wakapiga
stori.
“Nampenda
Jokate kwa sababu mpole, anatoka katika familia ya wachakarikaji, hivyo
nimekuwa nikimshirikisha katika mambo yangu. Nampenda kwa sababu hiyo
ila huwezi kuamini, nilipotezana naye na baadaye tumekuja kukutana
tayari yeye ni maarufu na sikuwahi kumwambia chochote juu ya kumpenda
kwangu kwa kuwa tayari ana ‘boy friend’ wake.
“Jokate
naye anamjua mchumba wangu ingawa hajawahi kumuona. Kwa sasa
namchukulia kama dada yangu tu kwa kuwa hakuna popote ambapo nimewahi
kutoka naye kimapenzi hata kwa dakika moja zaidi ya kuwasiliana naye
kikazi. Mara kadhaa nimekuwa nikimtafuta hata kama ni usiku wa manane
nikiwa na jambo na huwa sisiti kumshirikisha,” alisema Millard.
Kwa
upande wa Jokate baada ya kufikishiwa taarifa ya maneno ya Millard
alishangaa, akasema yeye hajui chochote. Kwanza aliwekewa mtego kama
angeuingia kwa kuambiwa Millard amemtaja yeye kuwa ni mchumba wake,
akashtuka na kusema:
“Huh!
Kasema hivyo lini? Maana mimi sijasikia lolote na siyo kweli kama ni
mpenzi wangu na sijui kwa nini kaongea hivyo. Kwa kweli sijasikia wala
kuongea naye.”
Wolper
yeye alipoulizwa juu ya maneno ya Millard kwamba hawajahi kuwa karibu
kwa jambo lolote zaidi ya kuonana barabarani alishtuka:
“He! Ni kweli lakini. Hata mimi namwonaga tu. Hivi yupo kwani hapa Bongo? Sina koneksheni ya kitu chochote na yeye.”
Lulu alipotafutwa juzi, simu yake iliita kwa muda mrefu lakini hakupokea.
Kuhusu
Millard na Jokate, baadhi ya vyombo vya habari vimewahi kuripoti kuwa
wako karibu kiasi kwamba, maswali ni mengi kuliko majibu.
Kwenye
‘bethidei’ ya Millard iliyofanyika Januari 26, mwaka huu nyumbani
kwake, Ubungo Msewe jijini Dar, Jokate alishiriki kwa kumpelekea keki ya
‘kumuwishi’ ambayo ilizua utata.
Nkupamah blog




0 comments :
Post a Comment