Mkulima Msaka urais Atua Morogoro Kusaka Wadhamini

  Nkupamah blog

MKULIMA wa Kigoma anayewania kupitishwa na CCM agombee urais kwa chama hicho, Idelphonce Bilole, ametua mkoani Morogoro akiendelea kutafuta wadhamini katika mikoa 15 nchini, huku akisisitiza elimu si kigezo cha yeye kushindwa kuwania nafasi hiyo ya juu.
 
Bilole aliyasema hayo jana katika ofisi ya CCM Wilaya ya Morogoro ambapo alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kiongozi ni lazima ajue kusoma na kuandika na kwamba CCM ni chama pekee ambacho hakina ubaguzi.
 
Aidha, alisema mwaka 2003 alifuatwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wakimtaka ajiandae ili aweze kuwania nafasi hiyo kwa mwaka 2005 ambapo alisema alikubali na aliandika barua ya kuomba kuteuliwa, lakini kutokana na sababu ambazo yeye hakuzifahamu barua ile ilichelewa na hivyo kuamua kuvuta subira.
 
Hata hivyo alisema kuwa mwaka huu ameona ni muda muafaka wa yeye kuwania nafasi hiyo ambayo wanachama wenzake wamekuwa wakimuomba kugombea ambapo alisema kuwa ameshafika katika mikoa kadhaa ikiwemo Dodoma, Kigoma, Mwanza, Simiyu, Singida, Shinyanga, Geita na sasa Morogoro kwa ajili ya kutafuta wadhamini.
  Nkupamah blog
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment