Shamsa Ford: Dickson (ex wake) amewahi kunitishia kutuua mimi na mtoto zaidi ya mara 10


Thursday, June 25, 2015

 Nkupamah blog

Muigizaji wa filamu, Shamsa Ford amesema tangu aachane na aliyekuwa mume wake Dickson Matoke, amewahi kuwatishia kuwaua yeye na mwanae zaidi ya mara 10.

Shamsa alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV kuwa ex wake huyo alikuwa na matatizo mengi ambayo alishindwa kuyavumilia.
 
“Namshukuru baada ya kuwa gizani sasa hivi nipo kwenye mwanga. Dickson kanifanya nijifunze vitu vingi sana, vitu vingi vya kifamilia nilikuwa nafanya mimi kama mimi, yeye kazi yake ni kukesha baa anakunywa pombe na marafiki zake.Nimeshagombana na marafiki zake wote,” Shamsa alimwambia mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema.
 
“Kuhusu kumtaka mtoto huo ndo ugomvi wetu huwa tunagombana kila siku. Sababu ya kwanza kwanini namnyima mtoto wangu Dickson alishaonyesha roho mbaya kwa mtoto wangu na mwanamke yoyote ambaye una uchungu na mtoto wake huwezi kumuachia mtoto. 
 
"Dickson alitamka sio mara moja, siyo chini ya mara kumi, katamka kwangu, mbele ya ndugu zake , katamka kwa marafiki zangu kwamba ‘ipo siku nitakuja kumuua Shamsa na mtoto wake.’ 
 
"Hilo neno zito sana, yule mtu yupo desperate, hana kitu chochote cha kupoteza. Leo hii ninaweza nikampa mtoto akaona ‘huyu Shamsa huyu anaringa acha nimkomoe,’ akimuua mtoto wangu halafu yeye akaenda Segerea hana cha kupoteza, lakini mimi nitaumia sana.” aliongeza kwa uchungu.
 
Katika hatua nyingine Shamsa amekanusha kutoka kimapenzi na Nay wa Mitego na kudai kuwa bado hajafikiria kurudi kwenye uhusiano.
Nkupamah blog
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment