Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.
Msemaji
wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na
familia yake ,''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi
Mungu,tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha
upendo kwa miezi michache iliyopita''.
Bobbi
ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake
panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku
akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata
fahamu bado.Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake
Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitliza
kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufa.
Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B.
Chanzo: BBC Swahili
Chanzo: BBC Swahili



0 comments :
Post a Comment