Ofisa
Mtendaji wa Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda
Isaack, akisikiliza maoni kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea
banda la Kampuni ya MO Assurance lililopo ndani ya banda la MeTL Group
katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja
vya Mwl. J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Meneja
mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO, (MO ASSURANCE), Ravinshankar
Venkatrama (kulia) akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa
Makampuni ya MeTL Group, Hussein Dewji alipotembelea banda la MO
Assurance kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kutimu vumbi jijini
Dar.
Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group, Hussein Dewji, akipata
maelezo kutoka kwa kijana anayetoa huduma kwenye bidhaa za Sundries
zinazotengenezwa na kampuni ya MeTL Group. Kulia ni msimamizi wa duka la
bidhaa za Sundries, Sandeep Gaur alipotembelea maonyesho ya Sabasaba.
Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group, Hussein Dewji,
akisalimiana Meneja wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi (wa pili
kulia) alipowasili kwenye banda la bidhaa za LG ambapo kampuni ya
Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) ndio msambazaji rasmi wa
bidhaa hizo nchini.
Mfanyakazi wa kampuni ya 21st
Century Textiles Ltd, Hidaya Kapera akitoa ufafanuzi kwa wateja
waliotembelea banda hilo linalouza vitenge vya aina mbali mbali kutoka
kampuni za Afritex Ltd, Musoma Textiles Ltd na Novatexmoque ambazo zote
ziko chini ya MeTL GROUP.
Mfanyakazi wa kampuni ya 21st
Century Textiles Ltd, Regina Waitara, akielezea ubora wa vitenge na
mashuka yanayozalishwa na kampuni hiyo kwa mmoja wa wateja aliyetembelea
banda hilo.
Balozi
wa bidhaa za LG, Albert Laurent akitoa maelezo ya bidhaa za LG ambazo
zipo katika punguzo la bei la 15% katika msimu huu wa maonyesho ya
Sabasaba na mwezi mzima wa Ramadhan kwa wateja waliotembelea banda hilo
ndani ya viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere.
Wananchi
wakijipatia huduma ya vinywaji baridi vya MO vikiwemo MO Cola, MO
Portello, MO Embe, MO Chungwa sambamba na kinywaji cha MO BOMBA
kinachokuburudisha na kukupa nguvu wakati wote.
Wateja
wakiwa wamefurika kujipatia bidhaa za sabuni katika banda la bidhaa za
kampuni ya Royal Soap & Detergent Industries Limited lililopo ndani
ya banda la MeTL Group.
Mfanyakazi
wa kampuni ya Royal Soap & Detergent Industries Limited, Saumu
Hamza, akionyesha bidhaa tofauti za sabuni za unga zinazopatikana katika
banda hilo.
Wateja wakifurahia sabuni za wa kampuni ya Royal Soap & Detergent Industries Limited.
Wafanyakazi
wa kampuni ya Sundries chini ya MeTL Group, Shomu Bhergava (kushoto) na
Sandeep Gaur (kulia) wakitoa maelezo kwa mteja alitembelea banda lao
katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K.
Nyerere, barabara Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa bidhaa za LG, Balbina Gabriel akimwonyesha mteja bidhaa ya Microwave
ya kampuni ya LG aliyetembelea katika banda la MeTL Group kwenye
maonyesho ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mdhibiti
ubora idara ya sabuni za kampuni ya MeTL GROUP, Cuthbert Sangiwa Msuya
akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi juu ya ubora wa mafuta ya
kulainisha ngozi (Lotion) inayoyazilishwa na kampuni hiyo.
Wafanyakazi
wa duka la vifaa vya LG lililopo ndani ya banda la MeTL Group katika
picha ya pamoja na Msimamizi wa banda hilo Sakina Alloo (aliyepiga
magoti).
0 comments :
Post a Comment