Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile (wa kwanza kulia)akiongea na baadhi ya viongozi wa
Ofisi ya Hazina Ndogo (hawapo pichani) hivi karibuni alipowatembelea
watumishi hao mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Hazina Ndogo Lindi Kassim
Kobelo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile (kushoto) akisalimiana na Mhasibu
Hazina Ndogo Lindi
Gasper Kaluntu (kulia) mara baada ya kuzungumza na Wafanyakazi wa ofisi
hiyo hivi karibuni mkoani Lindi.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Dkt. Servacius Likwelile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
watumishi wa Ofisi ya Hazina Ndogo hivi karibuni mkoani Lindi.
(Picha na Eleuteri Mangi-Lindi)
………………………………………………………………
Watumishi wa Serikali wameaswa
kuwa na nidhamu ya matumizi bora ya rasilimali fedha ili kuleta ufanisi
na maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi wa mkoani Lindi na Taifa
kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile alipokuwa akiongea na
baadhi ya watumishi wa Ofisi ya wafanyakazi Hazina Ndogo hivi karibuni
mkoani Lindi .
“Matumizi ya fedha ni lazima
yaende sawa na ukusanyaji wa mapato yakiwemo mapato yasiyo kuwa na kodi,
inabidi Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri kuzingatia umuhimu hasa
katika kusimamia mapato na matumizi ya Serikali kwa kila kiasi kidogo
kinachopatikana” alisema Dkt. Likwelile.
Dkt. Likwelile amesema kuwa
Serikali inafanya mapitio ya Mkakati wa Kupunguza Umasikini Tanzania
(MKUKUTA) na kuhakikisha kuwa changamoto zilizokuwepo awali zinapatiwa
ufumbuzi ili kuleta tija na ufanisi.
Kwa upande wake Meneja wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Lindi alipokuwa akimshukuru Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali kwa niaba ya watumishi wa
Hazina Ndogo alisema kuwa watajitahidi kuzingatia maelekezo aliyoyatoa
ili kuleta tija na ufanisi katika sehemu zao za kazi.
Imetolewa an Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha
Mkoani Lindi
08/08/2015
0 comments :
Post a Comment