Spunda achukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais

NCCR.
Na Anitha Jonas
Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Bw.Hashim Rungwe Spunda amechukua fomu rasmi katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini.
Akikabidhiwa fomu hiyo na mmoja wa Afisa wa Tume hiyo Bw.Adam Nyando  leo jijini Dar es Salaam Bw.Spunda alisema lengo lake la kugombea nafasi hiyo ni kuwasaidia watanzania na kuwatumikia kwa uadilifu.
“Nafasi hii ni ya juu sana katika uongozi na inahitaji uwajibikaji na siyo kuweka tamaa za kujineemesha huku ukiwaacha wananchi ambao ndiyo walipa kodi katika mazingira magumu na bila maendeleo,pia nafasi hii siyo ya kulilia kuipata kwa nguvu”alisema Bw.Spunda.
Aidha  mgombea huyo aliipongeza Tume ya Uchaguzi kwa kuliendesha zoezi la uchukuaji fomu vizuri bila tatizo lolote pia ametoa wito kwa wagombea wengine watakaokwenda kuchukua fomu wazingatie masharti yaliyowekwa kwa ikiwemo wasindikizaji wachache na utulivu.
Mbali na hayo Bw.Spunda alishagombea nafasi hiyo ya Urais katika uchaguzi wa mwaka 2010 kupitia chama cha CUF na kushinda kwa asilimia moja (1%)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment