Ukawa Nzega wadai, Hawawataki Viongozi Wasiotaka Mabadiliko!


Na Bryceson Mathias, aliyekuwa Nzega.
WANACHAMA wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wa Majimbo ya Nzega kwa Umoja wao, Wamedai hawawataki Viongozi wa Umoja huo Wasiotaka Mabadiliko, ambao katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, wanarubuniwa ili watengeneze Bao la Mkono.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti, baada ya kuiona Barua Kumb. CDM/MK/TBR/UCH/006 ya 23/8/2015 yenye Kichwa, ‘Utekelezaji wa Agizo la Mwenyekiti Taifa’ na SMS za Vitisho, Wamemuonya Katibu wa Mkoa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alinasusa Mwakilima, wakidai,

“Kama ataendelea kuwapotosha na kuwatisha Makatibu wa Chadema (W) wakiuke Katiba ya Chadema na Maoni ya Kamati Tendaji za Majimbo; bila kujali Vyama vyao, Watamshitaki kwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, wakiwemo Viongozi wa Kanda hiyo wasio Waadilifu.

“Hatuwezi kumkubali Katibu au Kiongozi wa Kanda, anayewatisha Watendaji waadilifu wanaosimamia Katiba na Maslahi ya Chadema na Ukawa kwamba, ni Jeuri na wanayofanya yatawagharimu!. Wenye Uadilifu hawawezi kuitwa Wasanii na Wenye Dharau! Je ni halali anayekataa Bao la Mkono, aitwe Jeuri au Anadharau? Walihoji!

Naye Katibu wa Chadema(M), Mwakilima, alipoulizwa alikiri kuandika barua CDM/MK/TBR/UCH/006 ya 23/8/2015 kwenda Bukene, akimlazimisha Katibu wake amuengue Mgombea wa Chadema aliyepitishwa na Kamati Tendaji ya Jimbo, awekwe aliyeshinda Kura ya Maoni, hata kama alijitoa na Kujiunga na Chama Kingine, ambapo Katibu (W) alilikataa.

Alipoulizwa kwa nini asiombe Ushauri Chadema Taifa, Mwakilima alisema hawezi kusikiliza Maagizo ya Chadema Taifa kuhusu Utendaji huo, isipokuwa yeye anasikiliza Maaagizo ya Kiongozi wa Kanda, jambo lililopingwa na Wana Ukawa wakidai, wanawagawa kimakundi, na wanaudharau Uongozi wa Taifa.

Hata hivyo Mwakilima aliwatuhumu, Viongozi wa Wilaya kwamba wanakiuka Mgawanyo wa Majimbo, lakini Wana Ukawa nao kwa upande wao walimtuhumu Mwakilima na Uongozi wa Kanda, wakidai wamerubuniwa waweke Mtu dhaifu, ili Mgombea wa Chama cha Mapinduzi apite bila kupingwa, jambo alilokanusha akisema ni Upuuzi!.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment