Published @nkupamah blog
Wachezaji
watano kutoka katika kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 15
(U-15) wanaondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea nchini Afrika Kusini
katika klabu ya Orlando Pirates kwa ajili ya kufanya majaribio.
Vijana
hao wanakwenda katika klabu ya vijana ya Orlando Pirates kufanya
majaribo ambapo makocha wa vijana wa klabu hiyo watapata nafasi ya
kuwatazama katika mazoezi na michezo ya kirafiki.
Nafasi
hiyo imepatikana kufuatia mazungumzo ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi na
Rais wa klabu hiyo Irvin Khoza kuomba vijana hao kupata nafasi ya
kufanya majaribio katika klabu hiyo na endapo watafuzu, watajiunga na
timu ya vijana ya Orlando Pirates.
Msafara
huo wa wachezaji utaongozwa na Mkurugenzi wa Ufudndi wa TFF, Salum
Madadi ambaye atakua na vijana hao katika kipindi chote cha majaribio
nchini Afrika Kusini.
Wachezaji
hao ni Asaad Ali Juma (Zanzibar), Maziku Aman (Dodoma), Issa Abdi
(Dodoma), Kelvin Deogratias (Geita) na Athumani Maulid (Kigoma).
Shirkisho la Mpira wa Miguu nchini linawatakiwa kila la kheri vijana hao katika majaribio yao huko nchini Afrika Kusini
0 comments :
Post a Comment