Inasadikika watu 12
wamepoteza Maisha na wengine 28 wamejeruhiwa jana baada ya basi la New
Force kupata ajali Eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
barabara kuu ya Iringa- Dar es salaam
Akithibitisha kutokea
kwa ajali hiyo,Kamanda wa polisi MKOA wa IRINGA Peter kakamba amesema
kuwa basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T483 CTF
lililokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Tunduma limepata ajali eneo la
MAHENGE kwa kugongana na Roli aina ya Scania lililokuwa limebeba mbao
likitokea NJOMBE kwenda Dar es Salaam .
Amesema kuwa ajali hiyo imesababishwa na kupasuka kwa tairi la MBELE la loli,na baadae likakosa mwelekeo ndipo lilienda kugonga basi hilo na kuuwa watu 12 na kujeruhi 28.
Kamanda Kakamba Amesema kuwa maiti zimehifadhiwa katika hospital ya MKOA wa IRINGA,na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.

Kwa upande wa mganga
MKUU mfawidhi wa hospital ya MKOA wa IRINGA Dkt Mseleta Nyakiroto
amethibitisha kupokea maiti na majeruhi katika hospital hiyo na kusema
kuwa majira ya SAA tisa na nusu jana alipewa taarifa ya kutokea kwa ajali na
taratibu za kupokea majeruhi na maiti zikafuata.
Aidha mganga huyo amesema kuwa maiti zote bado
hazijatambuliwa na ndugu zao.
Aidha mganga huyo amesema kuwa maiti zote bado
hazijatambuliwa na ndugu zao.

0 comments :
Post a Comment