Nkupamah media
EU yaendelea kuibana kiuchumi Urusi kutokana na ushiriki wake katika mgogoro mashariki mwa Ukraine
Na RFI
Umoja wa
Ulaya, kama ilivyotarajiwa, imechukua uamzi Jumatatu hii wa kuongeza
miezi sita kwa vikwazo vyake vya kiuchumi dhidi ya Urusi, kwa tuma za
kushiriki katika mgogoro mashariki mwa Ukraine, kwa
mujibu wa taarifa
rasmi.
"Tarehe
21 Desemba 2015, Baraza la Ulaya (linalowakilisha nchi 28 wanachama wa
Umoja wa Ulaya) limeongeza muda wa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi
hadi Julai 31, 2016",ilisema taarifa hiyo.
Vikwazo
hivyo vilichukuliwa Julai 31, 2014 kwa kipindi cha mwaka mmoja "katika
kukabiliana na vitendo vya Urusi mashariki mwa Ukraine",taarifa hiyo
imeongeza.
Vikwazo hivyo vilikua viliongezwa muda wa miezi sita tangu tarehe 22 Juni mpaka Januari 31, 2016.
Uamuzi
huu uliyokuwa ukisubirirwa, mabalozi 28 wa nchi wanachama wa EU walitoa
makubaliano yao Ijumaa kwa ajili ya kuongezwa kwa muda huo.
Vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya vinalenga sekta kubwa ya uchumi wa Urusi, kama vile sektabenki, ulinzi na mafuta.
EU pia
imetoa majina ya baadhi ya viongozi wa Urusi na Ukraine wanaolengwa na
vikwazo vya kupigwa marufuku ya kusafiri katika nchi wanachama wa Umoja
wa Ulaya na kuzuia mali zao kutokana na kuhusika katika machafuko
yanayoendelea nchini Ukriane.(P.T)


0 comments :
Post a Comment