Mkurugenzi
wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini
Tanzania, Peter Malika akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
makabidhiano ya misaada kwa miradi ya maendeleo iliyodhaminiwa na UNCDF
Tanzania.
Naibu
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba akisoma hotuba yake wakati
wa kukabidhi hundi kwa mashirika binafsi na ya umma kwa ajili ya
kuendeleza miradi ya maendeleo.
Naibu
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (katikati) akimkabidhi hundi
bilioni moja na milioni sabini (1,070,000,000) Mkurugenzi wa Mji wa
Kibaha, Bi. Jennifa C. Omolo (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko
wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania,
Peter Malika.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Moshi, Bw. Jeshi Godfrey Lupembe (kushoto) akikabidhiwa
hundi ya shilingi milioni mia tano na tisa (509,000,000/=) na Naibu
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (kulia) pamoja na Mkurugenzi
wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini
Tanzania, Peter Malika.
Naibu
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa
Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini
Tanzania, Peter Malika wakiwakabidhi masisita hundi ya milioni miamoja
na saba (107,000,000/=) wa kwanza kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Umeme
wa Lupali, Sister Imakulata Mlowe na Sister Helga Silinu ambaye ni fundi
umeme katika mradi wa Lupali.
Mkuu
wa wilaya ya Ileje , Mh. Rosemary Senyamule (kulia) akipokea hundi ya
milioni mia mbili na milioni ishirini na sita (226,000,000/=) kutoka kwa
UNCDF iliyotolewa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Tamisemi,
Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo
wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia kwa makini kinachozungumzwa na baadhi ya viongozi.
Mkurugenzi
wa Mji wa Kibaha, Bi. Jenifa C. Omolo akitoa neno la shukrani kwa niaba
ya sekta za umma na sekta binafsi zilizopata msaada huo ili kuendeleza
miradi ya maendeleo hapa nchini.
Picha ya pamoja.
…………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
MFUKO
wa Maendeleo ya Mtaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) umetoa msaada wa
shilingi bilioni 2.4 kama kianzio cha mtaji kwa waandaaji wa miradi
kutoka sekta binafsi na umma. Katika hafla iliyofanyika leo na
kufunguliwa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Kagyabukama Kiliba hawala
sita zilikabidhiwa wawakilishi wa waendeshaji katika miradi
iliyotawanyika sehemu mbalimbali nchini.
Pamoja
na hawala hizo za bilioni 2.4 imo pia shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya
miradi yenye mwelekeo wa kibiashara inayoandaliwa na mamlaka za
serikali za mitaa nchini Tanzania. Miradi iliyopewa kianzio cha mtaji ni
pamoja na halmashauri ya mji wa Kibaha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha
basi na soko la kisasa, halmashauri ya manispaa ya Moshi kwa ajili ya
kituo cha kisasa cha mabasi cha biashara na manispaa ya Ileje kwa ajili
ya ujenzi wa mnara wa redio kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Mradi
mwingine ni wa uzalishaji wa umemejua (mtandao wa vijijini)
unaotekelezwa wilaya ya Korogwe na kampuni binafsi ya Ensol, mradi
binafsi wa uzalishaji umeme kwa maji unaoendeshwa na wanawake wa wilaya
ya njombe vijijini na mradi mdogo binafsi wa uzalishaji umeme wa Maguta
uliopo wilayani Kilolo. Akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hundi
hizo, Mkuu wa UNCDF nchini Tanzania Peter Malika alisema msaada
uliotolewa umelenga kuonesha mafanikio ya program ya mradi wa fedha za
nahalia (LFI) wa UNCDF katika kusaidia waandaaji wanaojishughulisha na
miradi inayotoa mchango katika maendeleo ya uchumi ya maeneo husika.
“Licha
ya kuongezeka kwa upatikanaji wa mtaji wa uwekezaji kutoka vyanzo vya
umma na binafsi kwa ajili ya miundombinu, ni kiasi kidogo sana
kinachofikia miundombinu ambayo inaunda uti wa mgongo wa michakato ya
uchumi. LFI ilibuniwa ili kushughulikia changamoto hizi na uliundwa ili
kuonyesha kwamba miradi ya miundombinu ambayo inapewa kipaumbele na
serikali za mitaa na jamii inaweza kuvutia fedha endapo matatizo ya soko
la mtaji yaliyopo yatashughulikiwa” alisema Malika.
Aidha
Malika alisema katika mwaka huu timu ya LFI ilitoa msaada wa kiufundi
wa kulenga na kianzio cha mtaji kwa zaidi ya miradi 30,tisa kati ya hiyo
ikiwa katika hatua za juu na kwa hiyo kuwa tayari kupokea uwekezaji
ikiwemo miradi tisa iliyotunukiwa msaada jana. Tangu kuanzishwa kwake
mwaka 2012 LFI-T imesaidia zaidi ya miradi ya maendeleo ya mahalia 30
nchini Tanzania katika hatua mbalimbali tangu uwekaji mipango hadi kuwa
tayari kupokea uwekezaji kwa kufanyakazi kwa karibu na Tamisemi na
taasisi za fedha.
Aidha
LFI-T inasaidia miradi katika mikoa 18 iliyo katika sekta mbalimbali
ikiwamo ya usindikaji mazao ya kilimo, tabia nchi, nishati salama na
uzalishaji wa bidhaa za viwandani. Naye Naibu Katibu Mkuu Kiliba
akizungumza na hadhara kabla ya kutunuku hawala hizo sita alisifu kazi
ya ubunifu iliyofanywa na UNCDF katika utoaji fedha kwa maendeleo ya
jamii na kusema hiyo ndiyo njia sahihi ya kusababisha maendeleo. Pia
aliwapongeza waanzishaji wa miradi walipookea kianzia cha mtaji wa
uwekezaji kutoka UNCDF na kuwatakia mafanikio mema huku akisema kwamba
serikali ya Tanzania inakaribisha uendelezwaji wa program ya
LFI-Tanzania.
Kiliba
alisema kwamba wizara yake imeanzisha kitengo maalumu cha kuhakikisha
kwamba miradi ya ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi katika
halmashauri inafanikiwa.Mmoja wa wakurugenzi wa halmashauri waliopewa
mtaji huo wa kianzio, Jenifa Omolo kutoka halmashauri ya mjui wa Kibaha
alishukuru UNCDF kwa kufanikisha halmashauri ya Kibaha kuwa na soko la
kisasa na kituo cha basi cha kisasa.
AlisemaUNCDF
na Tamisemi wamekuwa mstari wa mbele katika kuwezesha kutekelezwa kwa
wazo hilo kuanzia mwanzo hadi sasa wanapopata mtaji huo. Alihimiza
halmashauri nyingine nchini kupata msaada wa kiufundi kwa mawazo yao
kutoka UNCDF ili kuwa na uwezo wa kusimamia maendeleo ya umma na
jamii. “Hatuna soko katika mji wetu, kuna magenge tu na tuna kituo
kidogo tu cha mabasi ambacho hakikidhi mahitaji- hizi zimekuwa
changamoto kubwa kwetu kwa zaidi ya miaka kumi. Mji wetu unakua na sasa
tunahitaji kuwa na miundombinu ya kisasa” alisema Omolo na kuongeza kuwa
mji wa Kibaha una wajibu wa kutoa huduma bora na kwamba miundombinu
mipya na ya kisasa itasaidia kuongeza mapato kwa mji huo.


0 comments :
Post a Comment