Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini
jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu, John Mngodo. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliitaka
Idara hiyo ya Uhamiaji kuanz rasmi kwa operesheni ya kuwakamata
Wahamiaji Haramu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi wanaosubiri
kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya
Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara
ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza kazi mbalimbali
zinazofanywa na Uhamiaji. Katika hotuba yake, licha ya maelekezo mengine
aliyoyatoa kwa viongozi wakuu, pia aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji
kuanza rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Afisa Uhamiaji anayeshughulika na
uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo
ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ambaye alifanya ziara ya
kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi
Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara
ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo,
Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Sylvester Ambokile akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya
kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (wasita kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo (wanne
kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Idara ya
Uhamiaji wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya
Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wasita kushoto ni Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments :
Post a Comment