Mwanasiasa Mmmoja Nchini Ujerumani ..........Apendekeza wanaoingia Nchini Humo bila Idhini wapigwe risasi.

  • Nkupamah Media:
Image copyrightAP
Image captionApendekeza wakimbizi wapigwe risasi Ujerumani
Mwanasiasa mmoja mbishi nchini Ujerumani ameibua hasira kubwa, baada ya kupendekeza kuwa maafisa wa polisi wanafaa kuruhusiwa kuwapiga risasi wahamiaji, wanaojaribu kuingia nchini humo bila idhini.
Kiongozi mkuu wa chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany Frauke Petry, ameliambia gazeti la Mannheimer Morgen, kwamba anapendekeza matumizi
ya silaha kwa polisi kama hatua ya mwisho.
Image copyrightReuters
Image captionFrauke Petry, wa chama cha Alternative for Germany ameliambia gazeti la Mannheimer Morgen, anapendekeza matumizi ya silaha
Sheria za polisi wa Ujerumani zinasema kuwa hakuna sheria inayodhinisha kushambulia wakimbizi kwa risasi.
Mwanachama mmoja mkuu wa chama cha Social Democrats, amemkumbusha Frauke Petry kwamba, mwanasiasa wa mwisho wa iliyokuwa Ujerumani mashariki, ambaye alimuru wakimbizi kupigwa risasi, alikuwa Erich Honecker, kiongozi mkuu wa utawala wa kikomunisti ambao ulisambaratika mwaka 1989.
CHANZO:BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment