Jac Wolper na Mkongo Wake Watimkia Sauzi Afrika.....


Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper na mpenzi wake Mkongo, wamedaiwa kuuza magari yao na kutimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.


Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina, kimepenyeza ubuyu kuwa miezi kadhaa iliyopita, maisha ya Wolper na Mkongo huyo yalibadilika na kuwa magumu hivyo katika kusaka suluhisho la kujikwamua, wakaamua kuuza magari yao na kwenda kuanzisha maisha mapya Sauz.

“Jamani mambo hapa kati hayakuwaendea vizuri Wolper na mpenzi wake hivyo waliamua kutimkia Sauz lakini waliuza magari yao na kwenda kuendelea na maisha mengine huko maana Mkongo alikuwa pia na makazi kule,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuinyaka habari hiyo gazeti hili liliwasiliana na Wolper kwa njia ya simu ambapo alikiri kuwa yupo Sauz na mpenzi wake Mkongo lakini akakana vikali suala la wao kuuza magari.

“Jamani kwa nini watu wako hivyo mimi sijauza gari langu lolote kama huamini nenda nyumbani utayakuta watu wanapenda sana kuzungumza vitu ambavyo hawana uhakika navyo kabisa.

“Tuliamua tu na mpenzi wangu tubadili maisha, tuhamie huku Sauz na si kwamba maisha Bongo yalikuwa magumu,” alisema Wolper.

Chanzo:GPL
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment