Nkupamah Media:

Mwana dada huyo ambaye jina lake la kisanii anaitwa Nandy na limetokana na jina lake la Nandela.Alishiriki kwa mara ya kwanza mnamo mwezi October 2015 katika Hotel moja hapa Dar es salaam ambapo walikuwa wakisakwa wasanii watano watakao iwakilisha Tanzania nchini Nigeria.Katika hatua hii kulikuwa na wasanii zaidi ya 50 na akafanikiwa kutinga tano bora.Wengine waliotinga tano bora ni pamoja na Zuchu,Kechu,Banye na Kandi Jefu.
Mashindano haya yanashirikisha nchi 3 yaani Kenya,Tanzania na wenyeji Nigeria,ambapo katika hatua 12 za mchujo Zechu,Kechu,Banye na Jefu toka Tanzania wamotolewa ktk mashindano,pia katika hatua hiyo ya fainali Wakenya 2 na Mnaigeria mmoja wamebakia ktk fainali hiyo,huku Tanzania ikiwakilishwa na msanii Faustina Charles a.k.a Nandy ambapo amekwea pipa leo kuelekea nchini Nigeria.Kila lakheri Nandy katika fainali hizo Watanzania wapo nyuma yako.Kumpigia kura Nandy nenda kwenye tovuti hii http://tecnoownthestage.com/vote/
0 comments :
Post a Comment