Nuhu Mziwanda Afikwa na Maji Shingoni...Ampigia Shilole Magoti

Nkupamah Media:

STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane. Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika
wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani. “Ndugu yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea na Shilole
akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu  alimtafuta Shilole kwa nia njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo ila hawezi kuanika wazi. “Suala la Nuh kwa sasa
sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana. Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment