Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai akizungumza na wabunge wa Bunge la
Afrika Mashariki (EALA) hawapo pichani kutoka Tanzania wakati
walipomtembelea katika ofisi zake zilizopo jijini Dar es salaam na kumpa
salaam maalum za kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa
kuchaguliwa kwake na watanzania na kuwa Rais wa Tanzania awamu ya Tano
ikiwa ni pamoja na kupongeza utendaji kazi wake kwa ujumla wake.(PICHA
NA Nkupamah media-DAR ES SALAAM)
Baadhi ya wabunge wa bunge la
Afrika Mashariki waliomtembelea Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kutoka
kulia ni Mh. Adam Kimbisa, Mh. Shy Rose Banjhi na Mh. Abdallah Mwinyi
wakizungumza na Spika wa Bunge.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai kulia akizungumza na wabunge hao.
Mkurugenzi wa Mhusiano ya Kimataifa ofisi ya Bunge Bw. Josey Mwakasyuka akijitambulisha katika mkutano huo.
Mh. Shy Rose Banjhi akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Spika wa Bunge Mh. Job
Ndugai kushoto ni Afisa habari wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya.
0 comments :
Post a Comment