Waziri
Mkuu. Mhe. Kassim Majaliwa amemtembelea Mwenyekiti wa CHADEMA na
kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe kumpa pole kufuatia kupata
kifo cha kaka yake Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe.
Mo Blog imekuandalia habari picha jinsi Waziri Mkuu alivyomtembelea Mbowe.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA na
kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe wakati alipokwenda kumpa pole
kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe,
nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha
kaka yake Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman
Mbowe (kulia kwake) wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha
kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa
marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wanafamilia wakati alipokwenda
kumpa pole Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman
Mbowe kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli
Mbowe,
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwanasiasa mkongwe nchini,
Kingunge Ngombale- Mwiru wakati alipokwenda kumpa pole Mwenyekiti wa
CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe kufuatia kifo cha
kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe,
0 comments :
Post a Comment