Kessy Amvaa John Mnyika......Asema Hapaswi Kumfananisha Profesa Muhongo na Edward Lowassa

Jina la aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa, jana liliingia tena katika Bunge la Kumi na Moja na kuzua mvutano.

Lowassa alitajwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), wakati akijibu hoja za Mbunge wa Kibamba, John Mnyika aliyekuwa akihoji na kuonesha kushangazwa na uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati alijiuzulu bungeni hapo baada ya kuelemewa na kashfa ya akaunti ya ‘Tegeta Escrow’.

Akijibu hoja hizo, Keissy ambaye siku zote ni mbunge mwenye hoja machachari alimvaa Mnyika  na kuhoji mbona wao ( UKAWA) walimchukua  Lowassa na kumfanya  kuwa mgombea wao wa Urais  wakati alijiuzulu uwaziri Mkuu kwa kashfa ya Richmond.

“Mnabeza  uteuzi wa Muhongo wakati Lowassa alivyojiuzulu hapa hapa bungeni mlimchukua mkamtembeza nchi nzima. Leo angekua Rais mgesema nini?" Alihoji Keissy .

Mnyika alikuwa alisoma hatuba ya kambi ya upinzani kwa Wizara ya Nishati na Madini ambayo ilikuwa ikiponda uteuzi wa Profesa Muhongo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment