Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetupilia mbali shauri la Msemaji wa Yanga, Jerry Muro kusikilizwa.
Kamati hiyo imesema hoja zilizotolewa ili kumuita Muro zilikuwa na mapungufu na haikuona kama kuna sababu ya kumuita na kumhoji.
“Kweli kamati ya maadili imetupilia mbali, ninaona ni ushindi kwa Wanayanga na ninawasamehe wote walionitesa.
“Huu
ni ushindi wa Wanayanga wote, lakini wito wangu kwa sasa ni sote
kuungana, kwa Wanayanga na TFF kwa ajili ya maendeleo ya soka nchini,”
alisema Muro katika ujumbe wake mfupi.
Jerry
aliitwa kwenye kamati ya maadili baada ya TFF kupitia katibu wake mkuu,
Mwesigwa Celestine kumtumia barua hiyo ya wito ingawa nayo ilikuwa na
mpungufu rundo kwani haikueleza hata anatakiwa katika kamati ipi.



Blogger Comment
Facebook Comment