Mlezi na mnazi mkubwa wa Wekundu wa Msimbazi Simba Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘MO’ amenogesha tamasha la timu kwa hali ya juu ambapo kila wakati wa mashambulizi baadhi ya mashabiki walikuwa wakiimba na kutaja jina la MO.
MO ambaye hadi sasa ameonyesha nia ya dhati ya kuitumikia klabu hiyo kama mfadhili mkubwa wapo katika mazungunzo ya hatua mbalimbali kufikia hali hiyo.
Timu ya Simba kaika mchezo uliomalizika hivi punde dhidi ya AFC Leopard, Wekundu hao waliweza kubadilisha mchezo wao kipindi cha pili baada ya Kocha wao kubadilisha safu ya ushambuliaji ndipo mabadiliko makubwa na kupelekea Simba kupata bao la 2 kupitia mchezaji wake Ibrahim Hajibu ambaye alitupia bao la kwanza kipindi cha kwanza na la pili katika kipindi cha pili tu cha mchezo huo.
Dakika mbili kadhaa za mchezo huo, Simba waliweza kufanikiwakupachika bao zingine 2, zilizotosha kabisa kunogesha mchezo huo maalum wa Simba Day pamoja na miaka 80 ya tokea kuzaliwa kwa timu hiyo ya Simba.
Katika mchezo huo ambao pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikuwa mgeni rasmi alipaa kulishwa keki sambamba na wadau wengine wakubwa wenye mapenzi mema ya Simba akiwemo Mbunge wa Nzega Vijijini na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla na Mlezi na mdau mkubwa wa Wekundu hao, Mh. Mohammed Dewji ‘MO’.
Mashabiki wa klabu hiyo baada ya mchezo walipongeza kikosi cha klabu yao hiyo kwa kuweza kufanya vyema katika mchezo huo ambapo licha ya kuwa mchezo wa kwanza na mkubwa mbele ya mashabiki wao, wachezaji wameonyesha hali ya juu ya kimchezo….
Mlezi na mnazi mkubwa wa Wekundu wa Msimbazi Simba Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘MO’ akilishwa keki ya miaka 80 ya Wekundu hao wa Msimbazi leo wakaati wa Simba Day , 8.8.2016
Mbunge wa Nzega Vijijini na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akilishwa keki hiyo ya miaka 80 ya Simba wakati wa tamasha la Simba day leo 8.8.2016
Wageni waalikwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, MO, na Dk. Kigwangalla wakitafakari jambo wakati wa tukio la kulishwa keki uwanjani leo wakati Simba Day .8.8.2016
MO akisalimiana na mashabiki wa Simba ambao muda mwingi walikuwa wakiimba na kulitaja jina la mfanyabiashara huyo ambaye ameonyeha nia ya kuwekeza kwenye Klabu hiyo..

Wageni waalikwa meza kuu akiwemo Hans Pop, Dk. Kigwangalla, MO,Aveva na Maakonda wakishangilia ushindi wa Simba mara baada ya Ibrahim Hajibu alipopachika bao la kwanza..
(Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).


0 comments :
Post a Comment