JESHI
la Polisi nchini linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya
kujichukulia sheria mkononi kuacha mara moja, kwani takwimu za makosa ya
kujichukulia sheria mkononi yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi
katika kipindi cha Januari hadi Agosti 2016 ni matukio 705.
Katika matukio hayo yaliyoripotiwa, Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 393.
Hayo
yametolewa katika taarifa kwa waandishi wa habari na Msemaji wa Jeshi
la Polisi Makao Makuu ya Polisi, ACP Advera Bulimba jijini Dar es
Salaam leo.
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa ni kosa kuzipuuza sheria za nchi zilizopo na wakati
mwingine kuzikiuka kwa makusudi na mbaya zaidi baadhi yao kufikia hatua
ya kuwaua watu wasio na hatia kwa hisia.
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa Mwananchi yeyote anapaswa kutoa taarifa kwa vyombo
vya dola ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mhalifu au
mtu yeyote wanayemtilia mashaka katika maeneo yao.
Aidha,
Jeshi la Polisi nchini, litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa
kufuatilia na kuwakamata watu wote wanaojihusisha na tabia za
kujichukulia sheria mkononi.
Jeshi
la Polisi linatoa wito kwa watu wote wakiwemo wenye ushawishi mkubwa
katika jamii kuendelea kukemea na kutoa elimu juu ya madhara ya
kujichukulia sheria mkononi



0 comments :
Post a Comment