Salum
Njwete maarufu kama ‘Scorpion’ anayetuhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa
macho, Saidi Mrisho amefikishwa mahakama ya Ilala Dar es salaam leo na
kusomewa shitaka la unyang’anyi kwa kutumia silaha.
Upande
mashitaka uliiomba mahakama kuliondoa shitaka la unyanganyi wa kutumia
silaha linalomkabili Salumu Njwete kwa nia ya kutotaka kuendelea nalo.
Kutokana
na ombi hilo hakimu Adelf Sachole alikubaliana na ombi hilo kuliondoa
shitaka hilo kupitia kifungu cha 91 (1) ambapo kinampa mamlaka
mkurugenzi wa mashitaka (DPP) kuondoa mashitaka muda wowote ilimradi
isifike kwenye hukumu.
Baada ya
saa kadhaa alifunguliwa shitaka hilohilo tena la unyang’anyi kwa
kutumia silaha alilolifanya September 6 2016 Buguruni sheli Dar es
salaam na jumla ya vitu alivyochukua 476000 kwa hakimu mwengine Frola
Haule. Salumu alikana mashitaka hayo.
Kutokana na kesi inayomkabili kisheria haina dhamana amerudishwa rumamde na kesi hiyo itatajwa tena November 2 2016



0 comments :
Post a Comment