Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la
Omega Ministry akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya
kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchungaji Samson
Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa.
Mchungaji Samson Shango Donalds
wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry.
…………………………………………………………..
Lilian Lundo, MAELEZO.
KANISA la Omega Ministry of All
Nations lenye makao yake Makuu Mbezi Afrikana, Jijini Dar es Salaam
limeandaa Semina ya Injili ya Neno la Mungu la kuiombea Taifa na
Viongozi wa Nchi, inayotarajiwa kufanyika Urafiki Nyangumi Jijini Dar es
Salam Octoba 21 mpaka 23 mwaka huu.
Nabii Samson Rolinga ameyasema
hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
kuhusu Semina hiyo yenye lengo la kuiombea Taifa, Viongozi wa Nchi na
kuwafungua watu katika vifungo mbalimbali.
“TutaliombeaTaifa lirudi katika
misingi ya Mungu, vile vile tutawaombea watu waliofungwa na nguvu za
giza na magonjwa kama vile kanda, ukimwi na utasa,” alifafanua Nabii
Rolinga.
Amesema magonjwa yapo lakini pia
yapo magonjwa ambayo yanatengenezwa na watu ilikumdhoofisha mtu, hivyo
katika semina hiyo kutafanyika maombi ya kuombea magonjwa hayo pamoja na
matatizo yote yanayotokonana roho za kurithi.
Vile vile amesema kuwa kumekuwa
na matatizo mengi sana ambayo watu hawana majibu ya matatizo hayo mfano
vijana wengi kutokuwa na kazi na kukata tama huku wakijraribu kupambana
na matatizo hayo kwa njia ya mwili.
Nabii Rolinga amesema kuwa lengo
lake nikuonyesha chanzo cha matatizo na kuyatatua kwa njia ya maombi
pamoja na kueleza namna ufalme wa giza unavyofanya kazi.
Kwa upande wake Nabii Donald
kutoka Mwanza amesema kuwa atakuwepo katika semina hiyo ambayo
itashughulikia matatizo ya Roho, kuvunja yanayoonekana katika ulimwengu
wa Roho pamoja na kuombea nchi na Utawala wa nchi.
Aidha amesema kuwa watumishi wa
Mungu wana jukumu kubwa la kuwaombea Viongozi wa Nchi na Rais ili Mungu
awasimamie katika majukumu yao ya kila siku ya kuliongozaTaifa.


0 comments :
Post a Comment