Mchezaji
wa Manchester United ambaye pia ndiyo mchezaji ghali zaidi kwa sasa
duniani, Paul Pogba amezungumza kuhusu uwezo wa soka ambao amekuwa
akionyesha uwanjani kutokana na kuwa akitupiwa lawama kuwa kiwango chake
kimeshuka.
Pogba
alisema kumekuwa na watu wakosoaji ambao wamekuwa wakimzungumzia uwezo
wake lakini yeye hajali na anadhani anahitaji muda ili kuzoea timu
anayoitumikia ya Manchester United.
“Nahitaji
muda kidogo kuizoea Manchester, muda ambao mashine itaanza kufanya kazi
nitakuwa nimezoea,” alisema Pogba wakati akizungumza na French TV na
kuongeza.
“Watu wanapenda kuzungumza kuhusu Pogba, ni wakosoaji kila siku, ila mimi sijali, naweka muziki na kucheza”


0 comments :
Post a Comment