Mwezi mmoja baada nahodha wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez kupishana maneno na Cristiano Ronaldo baada ya Ronaldo kusema hawezi kujilinganisha na Messi, mkongwe huyo amezungumzia nafasi ya Ronaldo kushinda tuzo ya Ballon d’Or.
Xavi amesema kwa uwezo ambao anaonyesha kwa sasa Ronaldo anaamini staa huyo wa Real Madrid ana nafasi ya kushinda tuzo hiyo kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa mwaka huu.
“Cristiano ana namba ya kushinda Ballon d’Or mwaka huu, ameshinda Ligi ya Mabingwa na Kombe la Euro akiwa na Real Madrid na Ureno,
“Lakini nafikiri jambo hilo litakuwa na ushindani mkubwa, kwasababu hata Messi yupo,” alisema Xavi.