Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua kianda cha kuunganisha magari ya zimamoto na matrekta cha
Equator SUMMA kilichopo Mlandizi mkoani Pwani Novemba 19,2016(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Kiluwa
Still Group cha Mlandizi mkoani Pwani Novemba 19, 2016. Kushoto ni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini
TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi wa reli inayounganisha
reli ya kati na kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi Pwani
Novemba 19, 2016 . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini
TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi wa reli inayounganisha
reli ya kati na kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi Pwani
Novemba 19, 2016 . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua mitambo ya kiwanda cha chuma cha Kiluwa Still Group kilichopo
Mlandizi Pwani Novemba 19,2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameliegiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha lifanye
maamuzi ya kupima ardhi haraka na kutenga maeneo kwa ajili makazi na
viwanda ili kujiandaa na uwekezaji mkubwa.
Ametoa agizo hilo leo mchana
(Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi
mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kukagua kiwanda
cha kutengeneza magari ya zimamoto na matrekta cha Equator SUMA JKT
Limited kilichopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
“Jiji la Dar es Salaam limejaa,
na Kibaha mjini pia hawana ardhi ya kutosha kwa kimbilio pekee hivi sasa
ni Kibaha Vijijini. Baraza la Madiwani fanyeni maamuzi, pimeni ardhi na
mtenge maeneo ya makazi, viwanda na taasisi za elimu ili mkipata
wawekezaji iwe rahisi kuwapa maeneo,” amesema.
Waziri Mkuu amesema ujenzi wa
kiwanda hicho utakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi na halmashauri nyingi
nchini kwani zilikuwa zinashindwa kumudu bei ya kununua magari ya
zimamoto. “Baadhi ya Halmashauri nyingi zilikuwa zinanunua gari moja kwa
sh. milioni 500 na hiki ni kiasi kikubwa mno… kwa hiyo kiwanda hiki
kitakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi na halmashauri zetu,” amesema.
Amesema maeneo mengi nchini
yanahitaji magari ya zimamoto lakini yalikuwa yanashndwa kumudu bei za
magari hayo. Aliyataja maeneo hayo kuwa ni viwanja vya ndege, bandari,
taasisi zilizo chini ya TAMISEMI kama vile shule za sekondari za bweni,
Majiji, miji mikuu, Manispaa na Halmashauri za Wilaya.
Amesema ameguswa kukuta kiwanda
hicho pia kina uwezo wa kutengeneza matreka na zana za kilimo (farm
implements) kwani asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima na
wanategemea jembe la mkono. “Kupitia kiwanda hiki, matrekta mengi
yataunganishwa na nina imani bei itakuwa ya chini ili wananchi waweze
kumudu.”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Equator SUMA JKT Ltd, Eng. Robert Mangazini alimweleza Waziri Mkuu
kwamba asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanda hicho imekamilika na kwamba hivi
sasa wako kwenhye hatua ya kufunga mitambo. Hata hivyo, alisema
wanaisubiri iwasili kutoka India.
Alisema kiwanda hicho
kikikamilika kitaweza kuunganisha matrekta 3,000 kwa mwaka na magari ya
zimamoto 100 na kubainisha kuwa faida za kuunganisha magari hayo hapa
nchini ni kuwa na uwezo wa kuzalisha vipuri ndani ya nchi.
“Tukiweza kuzalisha vipuri hapa
nchini kwa asilimia 60, umiliki wa magari haya na matrekta utakuwa ni wa
Tanzania na siyo wa kampuni za nje tena. Pia tutakuwa tumefaulu
kuhamisha teknolojia kwa vijana wetu,” alisema.
Alisema hadi sasa vijana 60 wamekwishapatiwa mafunzo ona wako tayari kuanza kazi mara uzalishaji utakapoanza Machi, 2017.
Kuhusu teknolojia ya utengenezaji
wa magari ya zimamoto, Eng. Mangazini alisema kiwanda hicho ni cha pili
kujengwa barani Afrika cha kwanza kikiwa huko Bassa, Afrika Kusini.
Mapema, akisoma risala mbele ya
Waziri Mkuu, mwakilishi wa Equator SUMA JKT Ltd. Kapteni Farijala
Mkojera alisema kiwanda hicho kinamilikiwa kwa pamoja na kampuni ya
Equator Automech Ltd ambao wana hisa asimilia 70 na SUMA JKT inamiliki
asilimia 30 ya hisa za kiwanda hicho.
Akizungumzia ujenzi wa kiwanda
hicho, alisema hadi sasa wamekwishatumia sh. bilioni 1.5 na kwamba hadi
ujenzi utakapokamilika, wanatajia kuwa wametumia sh. bilioni mbili.
“Ujenzi ukikamilika, tunatarajia kuajiri wafanyakazi 200 katika fani
mbalimbali,” alisema.
Alisema wakianza uzalishaji,
mbali ya magari ya zimamoto na matrekta, wataweza pia kuunganisha mabasi
na zana za kilimo kama vile combine harvesters. “Tutakuwa tumefanikiwa
kuhamisha teknolojia kutoka Russia (magari za zimamoto) na India na
Poland (matrekta). Tuna uhakika wa soko hapa nchini katika Jumuiaya za
EAC na SADC,” alisema.
Waziri Mkuu amerejea Dodoma mchana huu.


0 comments :
Post a Comment