Kocha
Mkuu wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ”amemeza kinga”
dhidi ya ukosoaji wa kupita kiasi, wakati ambapo timu yake inalenga
kuimarisha harakati zake za kushinda taji la ligi itakapokutana na West
Brom Albion katika siku kuu ya Boxing Dei.
Gunners wako katika nafasi ya nne
katika jedwali ,baada kushuka kwa alama tisa chini ya viongozi Chelsea
kufuatia ushindi wao dhidi ya Everton na Manchester City.
Wenger akiwa katika msimu wake wa 20 na Arsenal alifananisha soka na jamii pamoja na siasa akisema kila mtu ana maoni yake.
Je, Arsenal imeanza kupoteza pumzi
za kushinda taji? Raia huyo wa Ufaransa ,ambaye kandarasi yake
inakamiika mwishowe wa msimu huu amesema kuwa anaendelea kujiuliza kila
mara.
”Sina kinga dhidi ya ukosoaji” ,aliongezea ”lakini ukosoaji wa kupita kiasi ndio”.
”Nimehudumu kwa muda mrefu kwa
mimi kuhangaishwa na watu wanaopenda klabu hii ambao huwa wamekasirika
sana ifikiapo Ijumatatu asbuhi lazima tuwaelewe.Haimanishi kwamba
ahawatabadili msimamo wao tutakaposhinda mechi inayofuata”.
0 comments :
Post a Comment