Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewasili nchini kwao Ureno kwa ajili ya shughuli ya mazishi ya baba yake mzazi mzee Jose Manuel Mourinho Felix ambaye amefariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 79 baada ya miezi kadhaa ya kuugua.
Mourinho alionekana akiwasili Setubal akiwa na rafiki zake na familia yake Jumatatu baada ya taarifa za kifo cha baba yake cha baba yake mzazi ambaye atazikwa leo Jumanne.
Enzi za uhai wake na maisha ya soka, Mourinho Felix alikuwa mlinda mlango wa klabu za Vitoria Setubal kisha Belenenses akicheza mechi 274 za Ligi Kuu ya Ureno baina ya 1955 na 1974 huku akicheza mara moja pekee kwenye timu ya Taifa la Ureno akitokea kwenye benchi mchezo dhidi ya Jamhuri ya Ireland mwaka 1972.
Baada ya kustaafu soka Mourinho Felix alikuwa kocha wa klabu kadhaa za Ureno zikiwemo Uniao Leiria, Amora, Rio Ave, Belenenses na Vitoria.
0 comments :
Post a Comment