Baraza la taifa la usajiri wa zahanati binafsi na za umma wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto linamsaka daktari feki wa zahanati ya meno msasani jijini Dar es Salaam na kumburuza mahakamani kwa kugushi vyeti na vibali kinyume cha sheria huku akieleza wimbi kuanza kuota mizizi katika maeneo mengi nchini na wengine kutumia miavuli ya kijumuia.
Msajiri wa zahanati nchini Dk. Pamela Sawa sambamba na hilo pia ametaja makosa yaliyopo yanayobainika kwa baadhi ya zahanati binafsi kuwa ni pamoja na kuwa na mahabara zisizo na sifa stahiki kwa kutoa vipimo feki na dawa zisizoendana ugonjwa halisia huku baadhi yao kutumia watumishi wasio na sifa huku akishutumu mamlaka za manispaa na wilaya kupitia waganga wakuu wake kushindwa kusimamia sheria
0 comments :
Post a Comment