Licha ya kutoelezwa dhumuni la wito wote, kumekuwapo na tetesi ambazo hata yeye amekiri kuwa, huenda wito huo umetokana na kauli aliyoitoa mwishoni mwa juma kuhusu Masheikh wa Uamisho ambao wanashikiliwa na serikali kwa miaka minne sasa.
Akiwa katika futari hiyo aliyoalikwa, Lowassa alisema kuwa alipokuwa akigombea urais mwaka 2015, aliahidi kwamba, kama angeshinda, siku hiyo hiyo angewaachia viongozi hao wadini wanaoshikiliwa. Lakini kwa vile hakushinda, alimsihi Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo la viongozi wanaoshikiliwa kwa miaka yote hiyo bila kesi.
Mbali na hilo, Lowassa aliwataka waislamu kutokuwa wa baridi sana, badala yake watafute lugha
nyingine ya kuzungumza ambayo serikali itasikia ili kuachia viongozi wao wanaoshikiliwa.
Jambo hili huenda ndilo lililopelekea Lowassa kuitwa, kwani lina sura ya uchochezi ndani yake.
nyingine ya kuzungumza ambayo serikali itasikia ili kuachia viongozi wao wanaoshikiliwa.
Jambo hili huenda ndilo lililopelekea Lowassa kuitwa, kwani lina sura ya uchochezi ndani yake.
ITAZAME VIDEO HAPA CHINI
0 comments :
Post a Comment