Rais wa TFF Jamal Malinzi akipelekwa mahabusu pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa na viongozi wa Simba Evans Aveva na Geofrey Nyange.
Rais wa Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange wamepelekwa Rumande baada ya kukabiliwa na mashitaka matano ikiwemo ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana.
Washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutakatisha fedha ambayo ni dola za Marekani 300,000 walizozipata kwa kughushi nyaraka kuonesha kwamba Club ya Simba imelipa deni la fedha hiyo kwa Aveva.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema mashitaka hayana dhamana hivyo aliahirisha hadi Julai 13 mwaka huu kujua hatua ya upelelezi umefikia wapi.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema mashitaka hayana dhamana hivyo aliahirisha hadi Julai 13 mwaka huu kujua hatua ya upelelezi umefikia wapi.
Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa na Afisa wa fedha wa TFF Nsiande Mwanga wote kwa pamoja wamesomewa mashitaka ya jinai katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wanakabiliwa na mashitaka 28, katika mashitaka hayo Jamal Malinzi anakabiliwa na mashitaka zaidi ya 25 mengi yakiwa ni ya kughushi nyaraka katika michakato ya malipo mbalimbali.
Imeelezwa kwamba, kuna wakati Malinzi alikua anaandika risiti za kujilipa akidai kwamba aliikopesha TFF.
Lakini katika makosa hayo 28 kuna makosa matatu ya utakatishaji fedha yanawakabili, kuna kosa moja la utakatishaji fedha linalowakabili wote kwa pamoja. Kuna shitaka jingine linawakabili Malinzi na Mwesigwa huku kosa moja likimkabili Bi. Mwanga pekeake.
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka yanayo wakabili imeahirishwa hadi July 3, 2017 ambapo kutatolewa uamuzi kuhusu dhamana kwa watuhumiwa.
0 comments :
Post a Comment