JPM: asisitiza hakuna chakula cha msaada


Rais John Magufuli amesema Serikali yake haiwezi kutoa chakula kwa wananchi ambao wana uhaba wa chakula na kuwataka kuchapa kazi kwa ajili ya maendeleo yao.
Akizungumza wakati akiwa Wilaya ya Kankonko mkoani Kigoma, Rais Magufuli amesema kuwa jukumu la Serikali ni kuboresha miundombinu ikiwamo barabara na umeme.
“Inawezekana wengine walidhani Rais anawaletea chakula, siwaletei chakula ng’oo! Usipofanya kazi na usile na usipokula ufe. Ni lazima kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi na afanye kazi,” amesema.
Pia amewataka wafanyabiashara hasa katika vituo vya mafuta kulipa kodi. Magufuli ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa Barabara ya kutoka Kabondo hadi Nyakanazi inayogharimu Sh48.75Bilioni kwa bajeti ya Serikali
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment