Mfanyabiashara Yusuf Manji ameshindwa kwenda Mahakamani leo

Mfanyabiashara Yusuf Manji ambaye anakabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi leo July 19, 2017 ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na hali yake ya afya kutokuwa nzuri.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, Wakili mwandamizi wa serikali Nassoro Katuga àlidai amepata taarifa kutoka kwa Daktari wa Magereza kuwa Manji ni mgonjwa hivyo amepelekwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ‘JKCI’ iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Aidha, alidai Mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika lakini upo katika hatua ya mwisho hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi siku nyingine ambapo Hakimu Shaidi alikubali kuiahirisha kesi hadi August 4, 2017.
Hata hivyo Washtakiwa wenzake Ofisa Rasilimali watu, Deogratias Kisinda, msimamizi wa Stoo Abdallah Sangey na Msaidizi Mkuu wa Stoo Thobias Fwele wamefika Mahakamani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment