UN yashutumu jeshi la DRC kwa mauaji

Wapiganaji nchini DRC


WACHUNGUZI wa Umoja wa Mataifa wanaochunguza  mauaji ya wataalam wao nchini DRC wamebaini kwamba wanajeshi wa serikali ya hiyo wanahusika na mauaji hayo, anaandika Catherine Kayombo.
Awali, ripoti ya wachunguzi  hao kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa halikueleza moja kwa moja kwamba wanajeshi  hao wanahusika, bali imewaambia upelelezi unaendelea.
Wataalam hao wa umoja wa mataifa, Michael Sharp mwenye uraia wa Uswis na Zaida Catalan mwenye raia wa Chile waliuwawa mwezi Machi mwaka huu walipokuwa wakifanya utafiti kuhusu hali ya usalama nchini Congo.
Wakati huo huo, maofisa usalama nchini humo wanasema bado hawajafanikiwa kuwapata Mapadri wawili  wa Kanisa Katoliki waliotekwa na watu wasiofahamika.
Hali ya usalama nchini Congo DRC imeendelea kupungua huku serikali ya Kinshasa ikiwashutumu waasi wa Kamwina Nsapu kwa mauaji ya wataalamu hao.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment