Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuhamisha kituo cha kazi Christina Mndeme ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na sasa atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Mndeme ambaye awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, jana aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, alipangiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Jordan Rugimbana.
Akisema sababu ya uamuzi huo, Rais walisema kwamba, haiwezekani mtu akaazia Ukuu wa Wilaya Dodoma, halafu akipandishwa cheo kwenda Ukuu wa Mkoa aanzie tena Dodoma ambapo ni Makao Makuu ya Nchi.
Nataka aendeke kwanza Ruvuma akapate mitikisiko na kuhakikisha barabara zinajengwa, na wakati huko aliyekuwa Ruvuma atakuja Dodoma, alisema Rais Magufuli.
Aidha, Rais amesema kuwa viongozi hao walioapishwa leo wameanza kazi mara moja kwani hakuna suala la kuwa mgeni na yeye endapo atataka taarifa yoyote atampigia mtu simu amueleze licha ya kuwa ameapishwa leo, na hivyo ni lazima wajifunze vitu mbalimbali kuhusu maeneo yao
0 comments :
Post a Comment