Wakili Feki Akamatwa

Bw. Jeremiah Ragita aliyejifanya kuwa Wakili akitokea Kampuni ya Sheria ya Faithful Attorney Advocates kwa mujibu wa Naibu Msajili, Mahakama ya Ardhi, Mhe. Frank Mahimbali anasema Wakili huyo feki alikamatwa mapema Novemba 08 katika Mahakama hiyo akimsimamia Mleta maombi Nunu Mhusin Mkwata.
******
Mhe. Mahimbali anasema kuwa upande wa pili ambao unasimamiwa na Wakili Maros Gabriel kutoka Kampuni ya Sheria ya ‘Common Law Chambers’ ulimtilia shaka Bw. Jeremiah Ragita kama kweli ni Wakili ndipo alipofanya upekuzi kwenye Ofisi ya TLS na kuambiwa kuwa hawana jina hilo.

Hata hivyo Mhe. Mahimbali alienda mbali na kumuandikia barua Msajili wa Mahakama Kuu (RHC) na kujibiwa kuwa hakuna Wakili aliyesajiliwa kwa jina hilo.

Kwa mujibu wa Naibu Msajili kesi hiyo ilipoitwa mbele ya Mhe. Jaji Crencesia Makuru, Wakili Maros alimueleza Mhe. Jaji kuwa mwenzake wa upande wa pili sio Wakili na kisha akatoa vielelezo kutoka katika Ofisi ya Msajili Mahakama Kuu na Ofisi ya TLS ndipo Bw. Ragita akakiri kuwa yeye si Wakili.

Hata hivyo Bw. Ragita alikamatwa na kupelekwa Polisi Kituo cha Kati (Central Police) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hatua stahiki za kisheria.

Mahakama inapinga vikali vitendo vya ulaghai (Mawakili feki, vishoka) vinavyofanywa na baadhi ya Wananchi kwa lengo la kujipatia kipato.

(Imetolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment