Mmoja Wa Wanafunzi Bora Kidato Cha Nne Atoa Siri Ya Kufaulu

Mwanafunzi  aliyeshika nafasi ya tatu kitaifa Anna Mshana kutoka shule ya wasichana ya Marian iliyoko Mkoa wa pwani amesema mtoto wa kike ana uwezo wa kufanya vizuri kimasomo kama atajituma zaidi  na kuacha uvivu.

Anna ambaye ameonekana mwenye furaha baada ya kushika nafasi hiyo ambayo hakuitarajia amesema  siri ya mafanikio yake ni kujituma na kujiongeza bila kutegemea kila kitu kutoka kwa mwalimu.

"Kwanza tulisikia asubuhi kuwa matokeo yametoka, na tukaambiwa kuwa tumefaulu vizuri na shule yetu imeingia katika kumi bora, lakini furaha iliongezeka zaidi nilivyoambiwa kuwa nimekuwa wa tatu kitaifa," amesema.

Amesema ndoto yake ni kuwa mhandisi kwani mbali na kuwa alisoma masomo yote lakini alibobea zaidi katika masomo ya sayansi.

Amesema pia mafanikio yake kimasomo yametokana na jitihada pamoja na sala kwani hakuna mafanikio bila jitihada na kumtanguliza Mungu.

"Nilikuwa nafanya vizuri, lakini kutokana na msukumo kutoka kwa wazazi wangu imenifanya niwe nafanya vizuri kila siku, hivyo nilikuwa nasali kila mara," amesema.

Anna amewashukuru wazazi wake kwa ushirikiano wao mzuri, walimu na wanafunzi wenzake hata hivyo amesema matokeo hayo sio mwisho wa safari yake kwani ana safari ndefu kimasomo.

Mama mzazi wa Anna Zamara Hassani amesema matokeo hayo ni mwanzo mzuri kwa binti yao kwani jitihada zao ni kuhakikisha anasoma na kufaulu, vizuri masomo yake.

"Yaani tulifurahi sana, baada ya kusikia kuwa Anna ameshika nafasi ya tatu kitaifa, tulikuwa tunajua kuwa atafaulu lakini hatukuwaza yeye kuwa watatu," amesema.

Baba mzazi wa Anna Benjamini Mshana amesema amefurahishwa na matokeo hayo hivyo amemtaka binti yake kuongeza juhudi zaidi.

"Mzazi ukimsimamia vizuri mwanao ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri, mimi ni mwalimu najua umuhimu wa mzazi kumsimamia mwanafunzi kwani yeye hawezi, kujisimamia mwenyewe," ameongeza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment