Kesi inayomkabili aliyewahi kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ya kuhujumu uchumi imeahirishwa mpaka Feburuary 22, 2018 ya mwaka huu.
Chanzo cha kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kutokana na DPP kushindwa kukamilisha kusaini hati ya mashtaka hayo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri ambaye anasimamia kesi hiyo ameutaka upande wa Jamhuri kuhakikisha hati hiyo inasainiwa mpaka kufikia tarehe hiyo ili kesi iweze kuendelea mahakakamani hapo.
Awali Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamekwisha kamilisha upelelezi wa kesi hiyo inayowakabili viongozi hao wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
0 comments :
Post a Comment