Simba Yaendelea Kugawa Dozi



Klabu ya Simba leo imeibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Azam FC mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Bao la Simba SC limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi kunako dakika ya 37 kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo hayo Simba SC inaongoza katika msimamo wa ligi  kwa kuwa na jumla ya pointi 41 na kuweka rekodi ya kutopoteza hata mchezo mmoja mpaka sasa nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga SC wenye alama 33.

Katika michezo mengine iliyopigwa hii leo, Katika dimba la Majimaji mjini Songea, mchezo umemalizika kwa suluhu. Majimaji FC 0-0 Tanzania Prisons

Wakati huko CCM Kambarage mjini Shinyanga, Lipuli FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United.

Huko katika dimba la CCM Kirumba, Singida United wameondoka na pointi zote tatu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC.

ANGALIA GOLI LA OKWI HAPA CHINI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment