Familia ya Abdul Nondo Yakata Tamaa Baada ya Kushindwa Kumuona Tangu Ashikiliwe na Polisi


Imeelezwa kuwa familia ya  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo imeanza kukata tamaa  juu ya hatma ya mtoto wao baada ya kushindwa kumuona kwa zaidi  ya siku 10 tangu ashikiliwe na Jeshi la Polisi.
Hayo yamesemwa na Wakili wa mwanafunzi huyo, Jebra Kambole  wakati akizungumza na www.eatv.tv ambapoameweka wazi kuwa familia ya Nondo imeanza kurudi nyuma katika kumtafuatilia kijana wao na kwamba aliyebaki na moyo wa kumtafuta kijana huyo ni baba mzazi tu.
Wakili Kambole amesema kuwa Baba yake Nondo ndiye ambaye amekuwa kwa sasa wakihangaika naye kufahamu ni wapi Nondo alipo huku mzazi huyo akisema anamuomba Mungu kijana wake aonekane ili wafahamu shida ni nini.
Kwa upande mwingine Kambole amesema kuwa tukio la Nondo kutoonekana katika vituo vya polisi linamshangaza sana na hii imekuwa mara yake ya kwanza kukutana nalo tangu aanze kufanya kazi hiyo.
Mwenyekiti huyo wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha usiku wa Machi 6 na kesho yake machi 7 kujikuta Iringa na baada ya kuripoti kituo cha polisi mkoani huko alisafirishwa mpaka polisi Kanda Maalum Dar es salaam.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment