Haji Manara Aingilia Kati Sakata la Diamond na Naibu Waziri

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amefunguka na kumkingia kifua msanii Diamond na wenzake ambao wamekuwa wakitetea haki zo kwa Naibu waziri ambae ameibuka na sera ya kuwafungia wasanii kwa madai kuwa wanaimba nyimbo zisozokuwa na maadili katika jamii.

Hivi karibun Diamond aliongea katika media moja na kusema kuwa hata kama atatakiwa kulala jela kwa sababu ya muziki basi atafanya ilimradi kutetea haki ya muziki kwa sababu watu wanaofungia muziki huo hawajui historia ya muziki wala msanii wanaemfungia.

Haji Manara amesema  kuwa pamoja na kwamba wasanii wanaweza kuwa wamefanya kosa lakini wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la pili na kwa upande wa Diamond ni msanii mkubwa mbaye amekuwa akiiwakilisha nchi katika mambo mbalimbali.
 
"Ngoja na mimi nispitwe na hili..inawezekana kuwa kama binadamu anaweza kuwa amekosea , lakini inabidi tutambua kuhusu muziki wa kisasa na soko lake linataka nini..by the way diamond na wenzie tunawatumia sana katika maswala ya kijamii  na hata kampeni zetu za kisiasa,na huyu ni brand kubwa ,,,walau tufanye staha kidogo na tujitaidi tupende vya kwetu.

NB.mimi napenda muziki mzuri sina cha timu wala cha baba yake na timu….hawakawii wabongo. @diamondplatinumz"
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment