Leo March 20, 2018 moja ya stori ninayokusogezea ni kutoka Mahakamani ambapo Upelelezi wa kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa (TAKUKURU), Godfrey Gugai anayedaiwa kumiliki mali za Shilingi Bilioni 3 ambazo haziendani na kipato chake umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera.
Hayo yameeleza na Wakili wa TAKUKURU, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Vitalis amedai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika, hivyo anaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali (Ph).
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi April 10, 2018 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Kwa pamoja washtakiwa wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.
Gugai na wenzake wanasota mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
0 comments :
Post a Comment