Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka na kukiri haoni ubaya wa yeye kukata mauno stejini maana yupo kazini.
Suala limekuwa ishu baada ya video yake akiwa anatumbuiza stejini huku anakata mauno kihasara hasara stejini kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.
Ndipo watu kuanza kuhoji inakuwaje mke wa mtu anafanya mambo yake hadharani lakini Shilole amewazima watu hao na kusisitiza kuwa Mume wake anajua anachofanya hivyo haoni kama kuna tatizo.
Shilole amefunguka alipohojiwa na Global Publishers kuhusu hilo na kuweka wazi kuwa anawashangaa watu wanaozungumza kuhusu hilo wakati wanajua wazi kuwa ile ndio kazi yake na mume wake Uchebe analitambua hilo hivyo hana neno juu ya hilo.
"Mume wangu Uchebe (Ashraf) anajua nikiwa kazini, chochote naweza kufanya jukwaani, haoni shida maana ananipenda na kazi yangu hivyo wanaosema ninawasihi waache kwani pale nilikuwa kazini kwa hiyo lazima niwapagawishe mashabiki wangu
0 comments :
Post a Comment