Taswira ya Vijana Tanzania (TAVITA) Yalaani Wanasiasa Wanaochochea Uvunjifu wa Amani

Taswira ya Vijana Tanzania (TAVITA) imelaani vikali uchochezi unaofanywa na baadhi ya wanasiasa kupitia mitandao ya kijamii dhidi ya Serikali ya Awamu ya tano.

Akizungumza jana  jijini Dar es Salaam, Katibu wa TAVITA Otieno Peter alisema Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi kama vile kuanzisha miradi mikubwa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma.

Pia imejikita katika kusimamia rasilimali za nchi, kuhimiza uwajibika na kukomesha vitendo vya rushwa.Hivyo inasikitisha kuona baadhi ya watu wakitumia muda wao mwingi kuchochea uvunjifu wa amani badala ya kuelimisha jamii na endapo amani itapotea itakua imeharibu dira ya nchi yetu.

Ameviomba vyombo vya habari kutumia kalamu zao katika kuelimisha kuhusu masuala ya maendeleo kwa maslahi ya Taifa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa taasisi hiyo Shabani  Mwanga amewataka wananchi kutokubali taarifa zinazotolewa kwa ajili ya kuharibu taswira njema ya nchi kwani hao wanaofanya hivyo wanataka kuvuruga amani ya nchi iliyopo.

"Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mawakala ambao wanatumia saa 24 kutoa taarifa za kupaka matope ili kuharibu taswira njema ya taifa letu,"amesema .

Ameongeza taasisi ya Taswira ya Vijana Tanzania ipo tayari kupambana kwa hali yoyote na watu hawa wanaotaka kuchafua amani ya nchi na kwamba wapo tayari kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kwa maendeleo ya taifa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment