Yanga sasa kuja kidigitali

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa
KLABU Yanga imezindua kipindi cha televisheni kilichopewa jina la ‘Yanga TV Show’ sambamba na mfumo wa kuwapa habari wanachama wake utakaoitwa ‘Yanga Kidigitali’ vinavyotarajiwa kuanza Aprili Mosi Mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Kipindi cha Yanga TV Show kitakuwa kinarushwa kupitia kituo cha televisheni cha Azam TV wakati mfumo wa kutoa habari kwa wanachama wa Yanga Kidigitali utakuwa unapitia kampuni ya simu za mkononi za Tigo pamoja ya Prime.
Meneja wa michezo wa Azam Tv, Baruhan Muhuza amesema wameingia makubaliano na klabu ya Yanga ya uanzishwaji wa kipindi hicho baada ya majadiliano ya muda mrefu ili kufanya kipindi hicho kuwa cha tofauti.
“Yanga TV Show itakuja na muonekana mpya na wakipekee kwa kuwa itahusisha wachezaji wa zamani wa klabu hii kufanya uchambuzi katika michezo iliopita na itakayokuja katika Ligi Kuu pamoja na kuwajua mwenendo mzima wa timu inapokuwa ndani na nje ya Uwanja,” amesema Muhuza.
Aidha aliongezea ya kuwa Yanga kuwa na kipindi cha televisheni itakuwa fulsa kwa klabu katika kujiongezea mapato kwa kuwa kipindi kinaweza kupata wadhamini kutokana na kuwa cha tofauti na kufanya klabu hiyo iweze kujiendesha yenyewe kwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuanzisha Yanga TV Show na Yanga Kidigitali ni mikakati ya kuwapa fulsa wanachama wa klabu hiyo kupata habari za timu yao ikiwa pamoja na kujipatia kipacho ambacho kitaifanya waweze kujitegemea kwa kipato.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment