Na Kelvin Matandiko, Mwananchi
Posted Jumatano,Marchi19 2014 saa 13:54 PM
Posted Jumatano,Marchi19 2014 saa 13:54 PM
Kwa ufupi
- Sitta aliyechaguliwa kwa asilimia 86.5 ya kura za wajumbe wote, ana mtihani mzito aliobebeshwa mabegani ukiwamo wa kutetea msimamo wa chama chake au kuukan
Dar es Salaam. Mkanganyiko
pekee na uliobakia kwa Watanzania wakiwamo wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba ni viporo kwenye kanuni za 37 na 38, vinginevyo
hali ya hewa ndani ya Bunge hilo imetulia.
hali ya hewa ndani ya Bunge hilo imetulia.
Wajumbe wa Bunge hilo wapo tayari kuanza kibarua
cha kwanza cha kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya, kazi ambayo
hakuna shaka ndiyo iliyowaweka Dodoma.
Hata hivyo, kabla ya mwenyekiti mteule Samuel
Sitta kushinda kinyang’anyiro cha kuongoza Bunge hilo wiki iliyopita,
chama chake, CCM kimekuwa kikionekana kuwa na mkakati wa nguvu wa
kushawishi na hatimaye kupitisha mapendekezo na matakwa yake, yakiwamo
ya Serikali mbili.
Sitta ambaye amechaguliwa kwa asilimia 86.5 ya
kura za wajumbe ana mtihani mzito aliobebeshwa mabegani ukiwamo wa
kutetea msimamo wa chama chake au kuukana.
Akisaidiwa na Samia Suluhu Hassan ambaye naye amechaguliwa kwa asilimia 74, wawili hawa wana kibarua mbele yao.
Yeye (Sitta), ni muumini wa Serikali mbili kama
ilivyo CCM, ingawa inaaminika kuwa amebadili msimamo kutoka ule wa awali
wa Serikali tatu.
Tayari, ameahidi mbele ya wajumbe kulinda muungano kwa njia yoyote ile kupitia rasimu hiyo.
Mtego mpya kwake ndani ya Bunge ni imani kubwa
ambayo wajumbe hao wanayo kwake kwani bila kujali itikadi zao
wamempitisha kuwa mwenyekiti wao kwa idadi ya kura 487, sawa na asilimia
86.5.
Hii ni ishara ya kumwamini kwamba, atahakikisha anatetea masilahi ya Watanzania wote badala ya chama chake.
Matumaini hayo yanakuja baada ya kujijengea
uaminifu mkubwa kupitia uongozi wake wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya
Muungano kupitia kaulimbiu yake ya ‘kasi na viwango’.
Wapo Watanzania wanaosema kuwa nafasi hiyo kwa
Sitta inaweza kumjengea umaarufu ama kumwondolea imani kwao, endapo
hatakuwa mwangalifu katika kuliongoza Bunge hilo.
0 comments :
Post a Comment